Alhamisi 14 Agosti 2025 - 10:51
Darasa la Akhl'aq kwa wanaojiona wamekamilika

Hawza/ Utulivu wa nje wa mwanadamu katika hali ya kawaida mara nyingi huficha sura halisi ya nafsi; lakini hali zisizo za kawaida hufunua yaliyo ndani ya moyo, ni kama maji yaliyotuama ambayo yanapotikiswa, tope lililotulia chini hujitokeza – vivyo hivyo uchafu wa roho hujidhihirisha katika nyakati za misukosuko, hivyo basi, kujijua kwa hakika kuwezekana tu katika mitihani mikali ya kimaisha.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ustadh Shahidi Murtadha Mutahhari katika moja ya kazi zake ameelezea mada ya “uchafu wa roho”, ambayo tunaiwasilisha kwenu kama ifuatavyo.

Katika hali za kawaida, “uchafu wa roho” hujificha mbali na macho ya mtu.

Kwa ujumla, kila kitu kinachomweka mwanadamu katika hali isiyo ya kawaida na kuondoa utulivu wa nafsi, hudhihirisha tabia halisi ya mtu huyo.

Mwanadamu katika hali ya kawaida hufananishwa na maji yaliyotuama kwenye dimbwi.

Kwa sababu ya kutotikisika, mchanganyiko wa maji hutulia chini na maji huonekana safi na mang’avu.

Lakini pale tu unapotumbukiza mti ndani ya maji hayo na kuyatikisa na kuyachanganya, ndipo utaona ni kiasi gani cha uchafu kilichomo ndani ya maji hayo.

Wapo watu wengi ambao katika hali ya kawaida wanapoirejea nafsi yao huiona kama yale maji yaliyopo kwenye dimbwi yaliyo safi na tulivu.

Nao hawatambui kwamba pindi hali mpya ikijitokeza na sababu zikapatikana za kuibua sifa mbaya zilizokuwa zimetulia ndani, itadhihirika ni uchafu kiasi gani ulikuwa umejificha katika roho zao.

Chanzo: Ustadh Mutahhari, "Mchango kutoka Kitabu cha Hija", uk. 39

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha